NDEGE TAI
Tai ni ndege mbua wakubwa wa familia Accipitridae.
Wana makucha marefu ili kukamata uwimbo na domo kubwa lenye ncha kwa
kulabu ili kupapura nyama. Uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kabisa
na hutambua uwimbo kwa mbali sana. Tai hujenga tago lao juu ya miti
mirefu au magenge marefu. Pengine hutumika kwa uwindaji wa vipanga.
Sitapenda kumzungumzia sana huyu ndege ila napenda kuzungumzia sifa alizo nazo ambazo zinamfanya aonekane ndege wa mfano kuliko ndege wengine.Nadhani unafahamu kuwa Nchi ya Marekani inamtumia ndege huyu kama ndege wa Taifa (kwa Tanzania tunamtumia Twiga).
Sitapenda kumzungumzia sana huyu ndege ila napenda kuzungumzia sifa alizo nazo ambazo zinamfanya aonekane ndege wa mfano kuliko ndege wengine.Nadhani unafahamu kuwa Nchi ya Marekani inamtumia ndege huyu kama ndege wa Taifa (kwa Tanzania tunamtumia Twiga).
SIFA ZA TAI
Zifuatazo ni sifa za Tai,sio sifa zake zote ila ni baadhi ya sifa ambazo nimezipenda niweze kushea na wewe,angalau tumtumie ndege huyu kama mfano atusaidie kubadilisha maisha yetu na kufikia ndoto zetu.
- Utafiti unaonyesha kuwa ndege huyu anaona umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu.
- Anauwezo wa kuruka juu sana kuliko ndege wengine na kuona chakula kama vile samaki,kisha hulenga shabaa toka mbali na kumpata mlengwa.
- Huyu ni ndege mwenye nguvu kuliko ndege wengine.
- Huweka makazi yake juu ya miti mirefu sana kuliko ndege wengine.
Zipo sifa nyingi sana za ndege huyu ila sifa moja wapo niliyo ipenda ni JINSI NDEGE HUYU ANAVYO WEZA KUONA MBALI KUTOKA JUU KULIKO NDEGE WENGINE WOTE.Sifa hii ya ndege huyu ndio sifa inayo takiwa kuwanayo wewe na mimi kijana wa Kitanzania.Tunapaswa kuona mbali kama Tai,na maanisha tunapaswa kuona maisha yajayo na kujiandaa nayo sio kuona ya sasa au ya leo tu.Wewe kama kijana wa sasa tambua kwamba maisha yanaenda na UZEE unakaribia,hivyo usipo jiandaa na kupanga maisha yako ya baadae,utakuwa mzigo kwa familia yako,kwa jamii na kwa taifa yako pia.
Hebu na kuomba kijana wa kitanzania acha kufanya mambo ambayo yatakufanya ujekujutia hapo baadae,usihishi kufurahia maisha haya ya ujana tuu,angalia pia siku kama ya leo kesho utakuwa katika hari gani?Wajanja wanaenda na yote mawili wanafurahia ujana wao pia wanatengeneza vizuri maisha yao na wanauhakika wa kuishi maisha ya kheri hapo baadae.
Hivyo ushauri wangu kwako kijana wa kitanzania naomba tuwe na jicho la Tai katika maisha yetu tuishi kwa kufikiria mambo ya badae(watu wanasema kufikiria nje ya box),kama unawaza kuajiriwa na kuomba anza kuwaza kujiajiri.Tuache maisha ya kuiga na maisha ya kujionyesha(maisha ya usanii).Tupunguze muda wa kuchati tuongeze muda wa ujasiriamali.Kwanini ufe ombaomba au masikini wakati nguvu unazo sasa?
Tafadhari amuakufanya uamuzi wa faida,usiishi kizembe ONA MBALI,tumia nguvu zako za sasa kufurahia baadae.