KWA HABARI ZA SIKU BONYEZA HAPA!!!!!
Ndugu msomaji leo nimependa nikupatie
mada moja nzuri ambayo inaweza kukusaidia kuilinda Afya yako.Leo
nimependa kuzungumzia mada inayohusu MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA
HAUJATUMIA AU HAUJANYWA DAWA.Kabla sijakuambia mambo muhimu
unayopaswa kujua kabla ya kutumia dawa za kutibu maradhi ya mwili,ni
vyema ni kujuze maana ya Dawa.Huenda ukawa unafahamu maana nyingine za dawa ila hata hii ninayo kupa leo huenda ikafaa pia.Dawa ni kitu
au vitu vya kikemikali vinavyo tengenezwa na binadamu ndani ya
maabara au hutolewa katika vitu vya asili kama vile wanyama au
mimea,vinavyo tumika kujua ugonjwa,kutibu na kuzuia ugonjwa katika
mwili wa Binadamu.
Dawa hutumika kwa dhumuni maalumu la kuepusha mwili wa binadamu na maradhi au magonjwa kama vile,Malaria,Kichocho,Homa,Maumivu ya mwili,Taifodi,Ukimwi,Kisonono n.k.Na kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.
Watu wengi tumekuwa tunatumia dawa bila umakini wowote jambo ambalo tumekuwa tuki hatarisha maisha yetu wenyewe kwa kupuuzia tarifa muhimu za utumiaji wa dawa tupewazo.Jambo la muhimu kufahamu ni kwamba japo dawa hizi zinatumika kuzuia na kutibu maradhi ya mwili.Matumizi mabaya ya dawa hizi yanaweza kuadhiri miili yetu pia.Kumbuka kuwa dawa hizi ni kemikali hivyo matumizi mabaya ya dawa hizi yanaweza kufanya zikawa sumu kwetu na wala zisitusaidie.Baadae nitakuambia matumizi mabaya ya dawa ni yapi.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HAUJATUMIA DAWA
Yafuatayo ni mambo baadhi muhimu ambayo nimeona ni bora tushirikiane kufahamu, kabla ya kutumia dawa tunazo nunua au tunazopewa na madaktari au wafamasia na nurse.
- Kabla haujatumia dawa yoyote ni vizuri kwanza ujue unaumwa nini.Kila dawa imetengenezwa kwa ajili ya kutibu tatizo fulani katika mwili na ndio maana tunadawa tofauti tofauti,hivyo ni vizuri kabla haujatumia dawa yoyote kwanza jua ni nini tatizo.Na tatizo lako utalifahamu kwa kuenda katika vituo vya Afya na kupata vipimo maalumu kisha utapewa dawa sahihi.
- Zifahamu dawa vizuri dawa zako ulizopewa kwa kuomba maelekezo kutoka kwa mtoa huduma.Hii na maanisha fahamu jina la dawa zako na jinsi zinavyo weza kukusaidia.Hii itakusaidia kuwa na uhakika na moyo wa kutumia dawa zako vizuri kwa furaha bila wasiwasi wowote ukijua kuwa maradhi yako yataisha.Pia itakusaidia kutambua dawa zako endapo zitachanganywa na dawa za watu wa familia yako wanao tumia dawa.
- Hakikisha unajua jinsi ya kutumia dawa zako.Hapa maranyingi watu wanaopewa dawa huambiwa meza dawa kutwa mara mbili,au mara tatu au mara nne kwa siku,kwa siku kadhaa,kwa wiki au kwa mwezi.Na wao humeza kama walivyo ambiwa,unakuta mtu anakuambia nimeambiwa ni meze mara tatu kwa siku kwa hiyo nameza asubuhi,mchana na jioni.
SIKU MOJA INA MASAA 24 [ishirini na nne]
hivyo unapoambiwa:
- kunywa dawa mara mbili kwa siku anamaanisha tumia dawa yako kila baada ya masaa kumi na mbili.
masaa 24/2=masaa 12.
Hivyo dawa yako utakuwa unakunywa kila baada ya masaa kumi na mbili.Ambayo ni mara mbili kwa siku.
- Unapo ambiwa kunywa mara tatu kwa siku inamaanisha kila baada ya masaa nane tumia dawa yako.Unaweza pia ukatumia hesabu niliyo kupatia hapo juu pia.
- Unapo ambiwa kunywa mara nne kwa siku inamaanisha tumia dawa yako kila baada ya masaa sita.Pia waweza kutumia hesabu yetu kuhakikisha vizuri.
Unaweza kujiuliza swali je ni tajuaje kuhesabu masaa ya kunywa dawa zangu? Jibu ni rahisi unaanza kuhesabu masaa pale unapo kunywa dawa ya kwanza.Mfano kama umekunywa dawa sasa hivi, saa inayofuata hesabu kama ndio saa ya kwanza na kuendelea.
TAFADHARI
Zingatia sana maelekezo haya mpendwa ni mazuri kwa afya yako na itakusaidia kupunguza matumizi mengi ya dawa.[kwa taarifa zaidi kuhuhsu kipengele hiki fuatiria blogu hii]
- Hakikisha unajua madhara ya dawa uliyopewa ili kuepuka wasi wasi na kuacha kutumia dawa yako.Nime tumia neno madhara huenda ukawa umeshituka,ila usiwe na shaka yoyote.Unajua Mungu wetu ni waajabu sana kaumba miili yetu kwa mtindo wa ajabu sasa kulingana na maumbile ya kila mtu wapo ambao wakigusa,wakinusa au wakila au kunywa vitu fulani huwa wanapata madhara mfano kuwashwa,kubabuka ngozi na kadharika watu wenye sifa kama hizo huwa tunasema wanaalegi[alergy].Pia katika dawa tunazo tumia huwa kunaweza kukawa na kemikali ambazo hazipatani na mwili wako mfano SULPHUR.Hivyo nivyema ukafahamu mapema ili kuepuka madhara hayo.
- Kabla ya kutumia dawa hakikisha umenawa mikono kwa sabuni na maji safi kisha hakikisha imekauka,na tumia majisafi na salama unapo kunywa dawa.Kama utakuwa unafanya kinyume na hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe na unahatarisha afya yako mwenyewe.
- Hakikisha unajua jinsi ya kutunza dawa zako kwa kupata maelekezo kutoka kwa watoa huduma.Na hakikisha unafuata maelekezo.Pia kumbuka dawa zote ziwekwe mbali na watoto kuepuka madhara na zisiwekwe sehemu zinapoweza kupigwa na mwanga wa jua kwa muda mrefu ili kuepusha kuharibika kwa dawa na kupoteza ubora wake.
- Jua mahusiano ya dawa yako na chakula au vinywaji kama vile Maziwa,na pombe.Baadhi ya dawa ukimeza unaweza kunywa maziwa mfano ni dawa zile zinazo yeyuka mapema zinapokuwa kwenye sehemu ya mafutamafuta kama vile ALU dawa ya malaria.
MATUMIZI MABAYA YA DAWA
Watu wengi wamekuwa wanatumia dawa vibaya sana wanatumia dawa kwa mazoea.Wengi wakijisikia vibaya tu wanatumia dawa,wengine kichwa kikiuma kidogo tu wanatumia dawa.Kufanya hivyo ni kuhatarisha afya yako,matokeo hauta pata sasa ila hapo baadae.Nivyema kujua tatizo lako la kiafya ndipo utumie dawa.Si kila homa ni malaria hivyo epuka kutumia dawa za malaria kutibu homa.
Pia watu wengi huwa hawamalizi dawa wanazopewa,huwa wanatumia dawa pale wanapojisikia wapo hoi,wakijisikia vizuri huwa wanazitupa.Wasipopona huwa ndio walalamikaji wa kwanza kuwa dawa hazifanyi kazi.Tabia hii sio nzuri kabisa kama unayo rafiki acha.Maliza dawa unazopewa ili kuzuia maradhi mengine yanayo weza kujitokeza.
KUMBUKA
- Usitumie dawa ovyo na dawa ziwe suruhisho la mwisho la kutibu maradhi yako.
- Funga chombo cha kutunzia dawa baada ya kutumia dawa zako.Usiache dawa wazi kuepuka kupoteza ubora wa dawa.
- Dawa yako ni yako na walasi ya mwingine hivyo itumie vizuri kama inavyotakiwa kwa sababu inauwezo wa kuboresha afya yako.
- Tunza dawa ikutunze
NINA KUSAIDIA KUFIKIA MALENGO YAKO KWA KUJALI AFYA YAKO.JITHAMINI,JIPENDE NA JILINDE PIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni