Jumatano, 17 Juni 2015

CHIPS SIO SUMU ILA SASA!!!!!

Habari yako ndugu msomaji,naamini haujambo,na u mzima wa afya.Karibu katika makala hii ya siku ya leo.Leo nimeona vyema kuongelea kuhusu miongoni chakula tunachokipendelea sana kula, chakula hicho ni "CHIPS".Nadhani wengi na wewe ukiwa miongoni mwao tunafahamu CHIPS ni nini.Kwa hapa bongo tumeendelea hadi tuna aina za CHIPS,kama vile chips dume(hii ni aina ya chakula ambacho kina vipande vidogo vya viazi utamu,au vipande vya mihogo vilivyo kaangwa).

Nimeleta maada hii ili niweze kukufahamisha madhara ya hiki chakula ambacho wengi tunakipenda na hasa watoto wa kike.Huenda umewahi kuambiwa kwamba chips ni sumu,au umewahi kusikia kuwa chipsi zinamadhara.Najua ulipo sikia ulishituka na huenda ulipunguza kutumia chips lakini ulipoona hakuna madhara ukapotezea ukaendelea kutumia,, si kweli???Leo nataka kukupa ukweli kuhusu chips na ninakuomba baada ya kusoma ubadilike tafadhari.
CHIPS ninazoongelea leo nizile zinazo tengenezwa kwa kutumia viazi mviringo.


Kisayansi inasemekana kuwa viazi mviringo vina chemical inayojulikana kama "solanum glycoalkaloid" chemical hii ni sumu pale inapoingia katika mwili wa binadamu.Lakini Mungu mkubwa ameuumba mwili wetu kiasi kwamba sumu hiyo au chemical hiyo inapoingia ndani ya mwili haiwezi kuingia kwa haraka  ndani ya damu na kuleta madhara hivyo hukaa ndani ya tumbo kwa muda mrefu,Ikiwa ndani ya tumbo mwili hubadilisha ile chemical kutoka katika sumu kali na kupeleka katika hali ya sumu isiyo kali,na ili kuepuka madhara ya sumu hiyo katika mwili,chemical hiyo huondolewa kwa haraka sana nje ya mwili kwa kupitia njia ya mkojo na njia ya kinyesi.

"CHEMICHAL HIYO HUWEZA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA KAMA VILE KIFO. NA ILI MTU AWEZE KUPATA MADHARA YA SUMU AU CHEMICAL HIYO INABIDII MTU HUYO ALE KIASI KIKUBWA CHA VIAZI AU VIAZI VINGI SANA KWA WAKATI MMOJA"

Kutokana na ulaji wetu nivigumu sana mtu kupata madhara yanayotokana na chemical hiyo.Hivyo usijali tumia viazi kama chips kwa raha zako ila kumbuka ulafi ni mbaya kula kwa kiasi epuka unene kwasababu unene ni hatari kwa afya yako.


Kitu kibaya sana ni jinsi chipsi zinavyo andaliwa,kitu kinachoweza kutupatia madhara na ambacho ni hatari sana ni mafuta yanayo tumika katika kutengeneza chipsi hasa kwa zile chipsi za kununua magengeni.

Kuhusu mafuta.Kisayansi inasemekana kuwa mafuta haya yanayotolewa na vyanzo vya asili ambayo tunayatumia kwa afya au ambayo ni mazuri kwa afya zetu mfano mafuta ya alizeti,mzeituni,karanga,n.k.Huwa kichemical yanajulikana kuwa au yanatokea kama "unsaturated fats".Tabia moja wapo ya haya mafuta ni kwamba yanaweza kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine form hizo zinajulikana kama "CIS" na "TRANS".
mfano wa cis


 
mfano wa trans


Ili kubadilika kutoka form(mfumo) moja kwenda nyingine kiasi kikubwa cha joto kinahitajika.Kwa kawaida mafuta huwa katika form ya "CIS" ambayo kiafya haina madhara.Matumizi ya mafuta nyumbani ndio matumizi yanayo hitajika,Jinsi unavyo tumia mafuta hayo hayo mara kwa mara bila kubadilisha ndipo unapoongeza uwezekano wa mafuta kubadilika kutoka katika form moja kwenda nyingine.


Mafuta ya kibadilika kuwa kwenye form ya "TRANS" ni hatari sana kwa Afya mafuta haya huweza kuleta au kusababisha KANSA YA UTUMBO.


Wauzaji wa chips wanaweza kutuletea madhara katika afya zetu kwa sababu sio wote wanaobadilisha mara kwa mara mafuta wanayotumia.Wengi hutumia mafuta hayo kwa muda mrefu kiasi kwamba wengine hadi chipsi zao huonekana nyeusi.Baadhi huchanganya mafuta yakula na yatransformer ili kupunguza upotevu wa mafuta.Hii ni hatari sana,tuwe makini na Afya zetu na tupende miili yetu ili tuishi maisha marefu.

Ushauri wangu kwako ni kwamba kama itawezekana jaribu kupunguza matumizi ya chipsi za kununua,ikiwezekana nunua viazi vyako mwenyewe utengeneze chipsi zako. 

UPENDE MWILI WAKO

Ijumaa, 12 Juni 2015

RAFIKI YAKO NI NANI

Habari yako ndugu msomaji leo nimeona vyema niongelee kuhusu rafiki.Hivi Rafiki ni nani? Huenda ili neno huwa unalisikia kila siku au mara kwa mara.Wengi hujua kuwa rafiki ni mtu tu wa karibu,lakini neno rafiki lina maana kubwa zaidi na jinsi tunavyo lifahamu.Rafiki ni mtu unayemfahamu,unaye mpenda na kumuamini,anaweza kuwa wakike au wa kiume.Maisha yetu huwathiriwa sana na marafiki tulionao."Kuna msemo unasema niambie rafiki yako nikuambie tabia yako".Watu wengi tumekuwa tunachagua marafiki tukidhani huenda watatusaidia lakini tunajikuta mambo yetu yote tunayopanga yanaharibika kutokana na marafiki tulionao.Vijana wengi tumejikuta tumejiingiza kwenye tabia mbaya zisizofaa kutokana na marafiki tulionao.



  Ninamambo machache sana nataka tujulishane yanayoweza kutusaidia kuishi maisha mema ambayo hayawezi kuathiriwa na marfiki


     Najua unarafiki,huenda amekufanya umebadilisha tabia yako,au huenda yeye hanatabia njema.Kituchakufanya ili asiweze kubadili mwelekeo wa tabia yako usimruhusu atawale maamuzi yako.Jaribu kuwa na maamuzi yako usije mruhusu mtu akakutawala.Watu wengi hasa vijana tumejikuta tunapotea kwa kuruhusu marafiki zetu kututawala,kiakili na kimaamuzi pia.Hivyo njia nzuri ya kuepuka ushawishi mbaya wa marafiki jaribu kuwa na maamuzi yako mwenyewe,na ujitawale wewe mwenyewe."Acha wengine waige maisha yako na marafiki wapende jinsi wewe unavyo ishi". Ukiruhusu wewe kuwafuata wao utajikuta unapotea.


    Jaribu kuwa makini unapochagua rafiki,angalia tabia zake na angalia kama anaweza kukufaa katika kufanikisha malengo yako.Rafiki ananguvu kubwa sana katika kubadilisha maisha yako,hivyo jitahidi sana katika chaguzi za marafiki.





“Chagua marafiki wanaoshiriki maadili yako ili uweze kuimarisha na kuhamasisha kila mmoja katika kuishi viwango vya juu".Na“Ili kuwa na marafiki wema, kuwa rafiki mwema. …

“Unapojitahidi kuwa rafiki kwa watu wengine, usipuuze viwango vyako.”

Kama wewe nimiongoni mwa watu waliyo athirika na marafiki,unaweza kubadilika na kuishi maisha mazuri.Jaribu kutengana na marafiki anzakufanya maamuzi yako mwenyewe.Fanya uchaguzi upya,Naamini ukiamua utaweza.

 


Alhamisi, 4 Juni 2015

MIONZI ya simu za mkononi inaweza kuathiri maendeleo ya ubongo wa watoto walioko tumboni mwa mama zao, utafiti umeeleza.Utafiti huo umetaja madhara mengine ya mionzi ya simu za mkononi kuwa ni uharibifu wa manii, mimba, kupungua kwa nguvu za kiume, kupoteza kumbukumbu na kuzaa watoto watukutu.

Pia umeeleza kuwa matumizi kupita kiasi ya simu hizo, husababisha mtindio wa ubongo na upungufu wa udadisi kwa watoto tangu udogo wao.

Hata hivyo, utafiti huo uliofanywa na Shule ya Tiba na Dawa ya Chuo Kikuu cha Yale, Marekani na kuripotiwa na Gazeti la The Telegraph la Uingereza, umepingwa na watafiti wengine, wakisema haujakidhi baadhi ya vigezo ili kuuthibitisha.
Kiongozi wa jopo la utafiti huo, Profesa Hugh Taylor alisema utafiti huo ulioanzia kwa panya, baadaye ulithibitika kwa binadamu.

Profesa Taylor ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Sayansi ya Uzazi, alisema: “Tulikuwa na panya wenye mimba katika maboksi na tuliwawekea simu juu ya vichwa vyao. Panya tuliokuwa tumewaweka katika bwawa lile, nusu yao walikuwa wazima na nusu yao walikufa. Panya waliokuwa hai tuliwaacha wajifungue na baada ya kujifungua, tukaanza kutafiti watoto wao.”
“Panya ambao hawakuwa karibu na simu za mikononi walionekana kuwa werevu. Kumbukumbu zao hazikupungua ikilinganishwa na panya walioathiriwa na mionzi ya simu za mikononi ambao katika vipimo vya awali wakiwa tumboni, walionekana kuhangaika.”

“Panya hao wenye mimba waliowekwa kwa siku 17 katika boksi hilo na simu kupigwa mfululizo juu ya vichwa vyao, walizaa watoto watukutu na waliokosa kumbukumbu.”
Aliongeza: “Matokeo hayo yanaweza kutokea kwa binadamu pia. Mjamzito anayetumia simu ya mkononi muda mwingi, anaweza pia kuzaa taahira.”

Utafiti huo umebaini kuwa kati ya asilimia tatu na saba ya watoto wenye umri wa kwenda shule, wana tatizo la utukutu linaloweza pia kuathiri maendeleo yao kitaaluma. Alisema kiwango hicho kimekuwa kikiongezeka kwa asilimia tatu kila mwaka tangu mwaka 1997.

Profesa Taylor alisema anaamini kuwa simu za mikononi pia ni sababu ya baadhi ya watoto kukosa adabu na pengine kutokuwa makini katika mambo mbalimbali wanapokuwa watu wazima.

“‘Huu ni utafiti wa kwanza unaoonyesha ushahidi wa madhara ya mionzi ya simu za mkononi. Tumeonyesha kuwa matatizo ya tabia katika panya yalitokana na mionzi ya simu za mkononi waliyoipata wakiwa tumboni,” alisema Profesa Taylor na kuongeza:

“Kuongezeka kwa utovu wa nidhamu kwa watoto kunaweza kuwa sehemu ya madhara ya mionzi ya simu, ambazo mama zao walikuwa wakizitumia wakati wao wakiwa bado tumboni.”

Profesa Taylor alifanya utafiti huo kwa kuwachukua panya 33 wenye mimba na kuwaweka kwenye boksi lenye nyavu kisha kuweka simu juu yake. Simu hiyo ilikuwa ikiita mfululizo kwa siku 17.
Pia aliwaweka panya wengine 33 katika mazingira ya aina hiyo lakini hakuweka simu juu ya boksi hilo.
“Zaidi ya watu 160 waliofanyiwa utafiti wa aina hiyo pia walionekana kuwa na tofauti za kitabia ambayo inaweza kuhusishwa na utafiti huo.

Hata hivyo, Profesa Taylor alisema kuna haja ya kuendelea kufanya utafiti zaidi ili kubaini sababu ya mionzi hiyo ya simu kuathiri watoto walio tumboni mwa mama zao na namna bora ya matumizi ya simu kwa wanawake wajawazito.

Mtaalamu huyo anatarajia kuungana na wenzake akiwamo Dk Devra Davis, anayeongoza Shirika lisilo la Kiserikali la Mazingira na Afya la “Environmental Health Trust” kwa ajili ya utafiti zaidi kuhusu madhara ya simu.

Mwaka 2011, Shirika la Kimataifa la Afya Duniani linalojihusisha na uchunguzi wa kansa, lilidai kuwa mionzi ya simu inaweza kusababisha kansa na hivyo jopo hilo la madaktari linaendelea na utafiti zaidi.

Nchi nyingine duniani ikiwamo Ufaransa, ilipiga marufuku kwa kampuni za matangazo ya simu kwa watoto kutokana na hatari mbalimbali zinazoweza kuwatokea.

Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la ‘Scientific Reports’ wiki iliyopita
Lengo la utafiti
Ongezeko la matatizo ya magonjwa wa mishipa ya fahamu, matatizo mbalimbali ya ubongo pamoja na magonjwa ya akili, ni mojawapo ya mambo yaliyochagiza kufanyika kwa utafiti huo.
Dk Hugh alisema simu za mkononi hazina madhara kwa watu wazima kama inavyodaiwa na wengi, lakini ni vifaa vyenye kuleta athari kubwa kwa watoto walio tumboni.

“Matatizo yanayowapata watoto wa binadamu walio wengi hivi sasa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mtindio wa ubongo, mishipa ya fahamu inasababishwa na matumizi ya simu za mkononi kwa mama wajawazito pamoja na kukaa nazo jirani kwa muda mrefu.”

“Haijalishi mama anaongea na simu au la! Mionzi inapenya na kuleta madhara pia kusababisha kazi ya ukuaji wa mtoto katika ubongo kulegalega, wapo ambao wanalala na simu kitandani zikiwa zimewashwa... hii ni hatari zaidi labda iwe imezimwa,” anasema Dk Hugh.

Watalaamu Dar
Akizungumzia utafiti huo jana, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia wa Taasisi ya Mionzi Tanzania (Taec), alisema ni vigumu kuukosoa utafiti huo kwa sasa hadi hapo Shirika la Afya Duniani (WHO), litakapotoa tamko sahihi ingawa alisema mionzi ina athari kubwa kwa binadamu.

“Nilipata kusoma utafiti huo katika mitandao siku mbili zilizopita, ni utafiti ambao umewekwa wazi, kwa kweli hata mimi ulinishtua, lakini ni mapema kuzungumzia hilo kwa sasa. Kwani utafiti huo bado unakinzana kwa mambo mengi, licha ya kupingwa pia na baadhi ya wanasayansi.

“Nadhani ni muda mwafaka sasa kufanya uchunguzi kwa binadamu na si kutumia panya kama walivyofanya Chuo Kikuu cha Yale. Hata hivyo, jopo la madaktari pia wanatarajia kufanya kikao chao mapema wiki hii, labda tutapata maoni mapya.”

Alisema kwa kawaida mionzi ina madhara kwa binadamu, lakini bado kuna maswali mengi kwa wanasayansi duniani ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, hivyo inawawia vigumu Taec kutoa ufafanuzi wowote kuhusu athari hizo.

Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy alisema utafiti huo unaweza kuwa msaada mkubwa kwa nchi kama Tanzania ambayo hivi sasa ndiyo imechipukia katika matumizi ya simu za mkononi.

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *