Alhamisi, 23 Aprili 2015

MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA KABLA HAUJATUMIA DAWA

KWA HABARI ZA SIKU BONYEZA HAPA!!!!!



 
Ndugu msomaji leo nimependa nikupatie mada moja nzuri ambayo inaweza kukusaidia kuilinda Afya yako.Leo nimependa kuzungumzia mada inayohusu MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HAUJATUMIA AU HAUJANYWA DAWA.Kabla sijakuambia mambo muhimu unayopaswa kujua kabla ya kutumia dawa za kutibu maradhi ya mwili,ni vyema ni kujuze maana ya Dawa.Huenda ukawa unafahamu maana nyingine za dawa ila hata hii ninayo kupa leo huenda ikafaa pia.Dawa ni kitu au vitu vya kikemikali vinavyo tengenezwa na binadamu ndani ya maabara au hutolewa  katika vitu vya asili kama vile wanyama au mimea,vinavyo tumika kujua ugonjwa,kutibu na kuzuia ugonjwa katika mwili wa Binadamu.


    
      Dawa hutumika kwa dhumuni maalumu la kuepusha mwili wa binadamu na maradhi au magonjwa kama vile,Malaria,Kichocho,Homa,Maumivu ya mwili,Taifodi,Ukimwi,Kisonono n.k.Na kuufanya mwili kuwa katika hali nzuri.


 Watu wengi tumekuwa tunatumia dawa bila umakini wowote jambo ambalo tumekuwa tuki hatarisha maisha yetu wenyewe kwa kupuuzia tarifa muhimu za utumiaji wa dawa tupewazo.Jambo la muhimu kufahamu ni kwamba japo dawa hizi zinatumika kuzuia na kutibu maradhi ya mwili.Matumizi mabaya ya dawa hizi yanaweza kuadhiri miili yetu pia.Kumbuka kuwa dawa hizi ni kemikali hivyo matumizi mabaya ya dawa hizi yanaweza kufanya zikawa sumu kwetu na wala zisitusaidie.Baadae nitakuambia matumizi mabaya ya dawa ni yapi.


MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA HAUJATUMIA DAWA 



Yafuatayo ni mambo baadhi muhimu ambayo nimeona ni bora tushirikiane kufahamu, kabla ya kutumia dawa tunazo nunua au tunazopewa na madaktari au wafamasia na nurse.


  • Kabla haujatumia dawa yoyote ni vizuri kwanza ujue unaumwa nini.Kila dawa imetengenezwa kwa ajili ya kutibu tatizo fulani katika mwili na ndio maana tunadawa tofauti tofauti,hivyo ni vizuri kabla haujatumia dawa yoyote kwanza jua ni nini tatizo.Na tatizo lako utalifahamu kwa kuenda katika vituo vya Afya na kupata vipimo maalumu kisha utapewa dawa sahihi.
  • Zifahamu dawa vizuri dawa zako ulizopewa kwa kuomba maelekezo kutoka kwa mtoa huduma.Hii na maanisha fahamu jina la dawa zako na jinsi zinavyo weza kukusaidia.Hii itakusaidia kuwa na uhakika na moyo wa kutumia dawa zako vizuri kwa furaha bila wasiwasi wowote ukijua kuwa maradhi yako yataisha.Pia itakusaidia kutambua dawa zako endapo zitachanganywa na dawa za watu wa familia yako wanao tumia dawa.


  • Hakikisha unajua jinsi ya kutumia dawa zako.Hapa maranyingi watu wanaopewa dawa huambiwa meza dawa kutwa mara mbili,au mara tatu au mara nne kwa siku,kwa siku kadhaa,kwa wiki au kwa mwezi.Na wao humeza kama walivyo ambiwa,unakuta mtu anakuambia nimeambiwa ni meze mara tatu kwa siku kwa hiyo nameza asubuhi,mchana na jioni.
Kufanya hivyo ni makosa makubwa ndugu yangu.Ni muhimu kufahamu vitu hivi.
SIKU MOJA INA MASAA 24 [ishirini na nne]
hivyo unapoambiwa:
  • kunywa dawa mara mbili kwa siku anamaanisha tumia dawa yako kila baada ya masaa kumi na mbili.
ili kufahamu unaweza kufanya hesabu mwenyewe.Chukua masaa 24 na kisha ugawanye kwa mbili.
masaa 24/2=masaa 12.
Hivyo dawa yako utakuwa unakunywa kila baada ya masaa kumi na mbili.Ambayo ni mara mbili kwa siku.

  • Unapo ambiwa kunywa mara tatu kwa siku inamaanisha kila baada ya masaa nane tumia dawa yako.Unaweza pia ukatumia hesabu niliyo kupatia hapo juu pia.
masaa 24/3=masaa 8.

  • Unapo ambiwa kunywa mara nne kwa siku inamaanisha tumia dawa yako kila baada ya masaa sita.Pia waweza kutumia hesabu yetu kuhakikisha vizuri.
Unaweza kujiuliza swali je ni tajuaje kuhesabu masaa ya kunywa dawa zangu? Jibu ni rahisi unaanza kuhesabu masaa pale unapo kunywa dawa ya kwanza.Mfano kama umekunywa dawa sasa hivi, saa inayofuata hesabu kama ndio saa ya kwanza na kuendelea.

TAFADHARI

   Zingatia sana maelekezo haya mpendwa ni mazuri kwa afya yako na itakusaidia kupunguza matumizi mengi ya dawa.[kwa taarifa zaidi kuhuhsu kipengele hiki fuatiria blogu hii]


  • Hakikisha unajua madhara ya dawa uliyopewa ili kuepuka wasi wasi na kuacha kutumia dawa yako.Nime tumia neno madhara huenda ukawa umeshituka,ila usiwe na shaka yoyote.Unajua Mungu wetu ni waajabu sana kaumba miili yetu kwa mtindo wa ajabu sasa kulingana na maumbile ya kila mtu wapo ambao wakigusa,wakinusa au wakila au kunywa vitu fulani huwa wanapata madhara mfano kuwashwa,kubabuka ngozi na kadharika watu wenye sifa kama hizo huwa tunasema wanaalegi[alergy].Pia katika dawa tunazo tumia huwa kunaweza kukawa na kemikali ambazo hazipatani na mwili wako mfano SULPHUR.Hivyo nivyema ukafahamu mapema ili kuepuka madhara hayo.



  •  Kabla ya kutumia dawa hakikisha umenawa mikono kwa sabuni na maji safi kisha hakikisha imekauka,na tumia majisafi na salama unapo kunywa dawa.Kama utakuwa unafanya kinyume na hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe na unahatarisha afya yako mwenyewe.


  •  Hakikisha unajua jinsi ya kutunza dawa zako kwa kupata maelekezo kutoka kwa watoa huduma.Na hakikisha unafuata maelekezo.Pia kumbuka dawa zote  ziwekwe mbali na watoto kuepuka madhara na zisiwekwe sehemu zinapoweza kupigwa na mwanga wa jua kwa muda mrefu ili kuepusha kuharibika kwa dawa na kupoteza ubora wake.


  • Jua mahusiano ya dawa yako na chakula au vinywaji kama vile Maziwa,na pombe.Baadhi ya dawa ukimeza unaweza kunywa maziwa mfano ni dawa zile zinazo yeyuka mapema zinapokuwa kwenye sehemu ya mafutamafuta kama vile ALU dawa ya malaria.
Hizo ni baadhi ya mambo ambayo nimependa ufahamu kabla haujatumia dawa,nadhani utakuwa umepata elimu fulani itakayo kusaidia kujenga afya yako.


MATUMIZI MABAYA YA DAWA

    Watu wengi wamekuwa wanatumia dawa vibaya sana wanatumia dawa kwa mazoea.Wengi wakijisikia vibaya tu wanatumia dawa,wengine kichwa kikiuma kidogo tu wanatumia dawa.Kufanya hivyo ni kuhatarisha afya yako,matokeo hauta pata sasa ila hapo baadae.Nivyema kujua tatizo lako la kiafya ndipo utumie dawa.Si kila homa ni malaria hivyo epuka kutumia dawa za malaria kutibu homa.

    Pia watu wengi huwa hawamalizi dawa wanazopewa,huwa wanatumia dawa pale wanapojisikia wapo hoi,wakijisikia vizuri huwa wanazitupa.Wasipopona huwa ndio walalamikaji wa kwanza kuwa dawa hazifanyi kazi.Tabia hii sio nzuri kabisa kama unayo rafiki acha.Maliza dawa unazopewa ili kuzuia maradhi mengine yanayo weza kujitokeza.

KUMBUKA


  • Usitumie dawa ovyo na dawa ziwe suruhisho la mwisho la kutibu maradhi yako.
  • Funga chombo cha kutunzia dawa baada ya kutumia dawa zako.Usiache dawa wazi kuepuka kupoteza ubora wa dawa.
  • Dawa yako ni yako na walasi ya mwingine hivyo itumie vizuri kama inavyotakiwa kwa sababu inauwezo wa kuboresha afya yako.
  • Tunza dawa ikutunze
NINA KUSAIDIA KUFIKIA MALENGO YAKO KWA KUJALI AFYA YAKO.JITHAMINI,JIPENDE NA JILINDE PIA



































Jumamosi, 18 Aprili 2015

TAI





NDEGE TAI

Tai ni ndege mbua wakubwa wa familia Accipitridae. Wana makucha marefu ili kukamata uwimbo na domo kubwa lenye ncha kwa kulabu ili kupapura nyama. Uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kabisa na hutambua uwimbo kwa mbali sana. Tai hujenga tago lao juu ya miti mirefu au magenge marefu. Pengine hutumika kwa uwindaji wa vipanga.
Sitapenda kumzungumzia sana huyu ndege ila napenda kuzungumzia sifa alizo nazo ambazo zinamfanya aonekane ndege wa mfano kuliko ndege wengine.Nadhani unafahamu kuwa Nchi ya Marekani inamtumia ndege huyu kama ndege wa Taifa (kwa Tanzania tunamtumia Twiga).

SIFA ZA TAI 
Zifuatazo ni sifa za Tai,sio sifa zake zote ila ni baadhi ya sifa ambazo nimezipenda niweze kushea na wewe,angalau tumtumie ndege huyu kama mfano atusaidie kubadilisha maisha yetu na kufikia ndoto zetu.
  1. Utafiti unaonyesha kuwa ndege huyu anaona umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu.
  2. Anauwezo wa kuruka juu sana kuliko ndege wengine na kuona chakula kama vile samaki,kisha hulenga shabaa toka mbali na kumpata mlengwa.
  3. Huyu ni ndege mwenye nguvu kuliko ndege wengine.
  4. Huweka makazi yake juu ya miti mirefu sana kuliko ndege wengine.
Zipo sifa nyingi sana za ndege huyu ila sifa moja wapo niliyo ipenda ni JINSI NDEGE HUYU ANAVYO WEZA KUONA MBALI KUTOKA JUU KULIKO NDEGE WENGINE WOTE.Sifa hii ya ndege huyu ndio sifa inayo takiwa kuwanayo wewe na mimi kijana wa Kitanzania.Tunapaswa kuona mbali kama Tai,na maanisha tunapaswa kuona maisha yajayo na kujiandaa nayo sio kuona ya sasa au ya leo tu.Wewe kama kijana wa sasa tambua kwamba maisha yanaenda na UZEE unakaribia,hivyo usipo jiandaa na kupanga maisha yako ya baadae,utakuwa mzigo kwa familia yako,kwa jamii na kwa taifa yako pia.
     Hebu na kuomba kijana wa kitanzania acha kufanya mambo ambayo yatakufanya ujekujutia hapo baadae,usihishi kufurahia maisha haya ya ujana tuu,angalia pia siku kama ya leo kesho utakuwa katika hari gani?Wajanja wanaenda na yote mawili wanafurahia ujana wao pia wanatengeneza vizuri maisha yao na wanauhakika wa kuishi maisha ya kheri hapo baadae.
    Hivyo ushauri wangu kwako kijana wa kitanzania naomba tuwe na jicho la Tai katika maisha yetu tuishi kwa kufikiria mambo ya badae(watu wanasema kufikiria nje ya box),kama unawaza kuajiriwa na kuomba anza kuwaza kujiajiri.Tuache maisha ya kuiga na maisha ya kujionyesha(maisha ya usanii).Tupunguze muda wa kuchati tuongeze muda wa ujasiriamali.Kwanini ufe ombaomba au masikini wakati nguvu unazo sasa?
         Tafadhari amuakufanya uamuzi wa faida,usiishi kizembe ONA MBALI,tumia nguvu zako za sasa kufurahia baadae.

Alhamisi, 16 Aprili 2015

KARIBU KATIKA BLOG HII


 "ONA MBALI KAMA TAI"



Karibu katika blog hii,kufungua blog hii haujafanya makosa.Hapa utapata mambo mbalimbali kama vile:
               1.Mahusiano
               2.Elimu ya madawa na Afya kwa ujumla
               3.Masomo yanayo weza kubadili maisha yako
               4.Mada zinazo muhusu Mungu
               5.Na matukio mbalimbali unayoweza kufurahia

Na amini siku utakayo fungua blog hii hautatoka bure utakuwa umeongeza kitu fulani katika maisha yako.Nakuomba pale panapotakiwa ushauri tushauriane.Kabla haujaanza kutumia blog hii nakuomba ubadili maisha yako kwa kuona mbali kama ndege tai..

"kabla sija anza kuweka dondoo mbalimbali naomba ni kupatie sifa za Tai na tuangalie kutoka kwake tunajifunza nin" 

ACCOMPLISH YOUR GOALS

ACCOMPLISH YOUR GOALS

In order to accomplish your goals three things are required:

1.Setting goals
2.Getting started
3.Accomplishing your goals

                       Part 1 of 3:  Setting Goals

    1.Start working toward your goals today. Ask yourself, "What can I do today to get one step ahead, however small, closer to achieving my goals?" Write it down and start now. Taking the first step is arguably the most important step. You'll establish some much-needed momentum. This will make quitting both personally disappointing and strategically harder. In the words of Eleanor Roosevelt, "Do one thing every day that scares you."

    2.When you set goals,think about setting SMART goals. SMART is an acronym and mnemonic that provides a framework for thinking about goals.[1] Educators and coaches like to use this framework because it forces us to sit down and really design our goals intelligently so that they're ultimately easier to accomplish. SMART stands for:
        S – Specific (or Significant).
        M – Measurable (or Meaningful).
        A – Attainable (or Action-Oriented).
        R – Relevant (or Rewarding).
        T – Time-bound (or Trackable).

Fomu ya Anwani

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *